1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Volkswagen yakumbwa na kashfa

7 Julai 2005

Kampuni kubwa kabisa ya magari barani Ulaya Volkswagen imechafuliwa na madai kwamba wafanyakazi wake waandamizi walijiendekeza na hadaa,rushwa na safari za bandia kwa kutumia gharama za kazi.

Chombo cha habari cha Ujerumani kimedokeza kwamba wajumbe wa baraza la kazi la kampuni hiyo viganja vyao vililainishwa na bakshishi maalum kuwafanya wakubali sera za kampuni hiyo wakati wa mikutano ya bodi.Chini ya utaratibu wa Ujerumani wa kuwapa waajiri sauti kubwa katika mchakato wa kupitisha maamuzi ya kampuni nusu ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi imeundwa na wawakilishi wa baraza la kazi na vyama vya wafanyakazi.

Kashfa hii ya sasa imewapa fursa wakosoaji kuhoji utaratibu huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW