1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wakuu wa Ujerumani, Ufaransa na urusi wakosoa uamuzi wa Marekani wa kukatalia makampuni ya nchi hizo kushiriki katika ujenzi mpya wa Irak

10 Desemba 2003
Wakuu wa Ujerumani na wa Ufaransa wamekosoa uamuzi uliotangazwa jana na Marekani, kwamba makampuni ya nchi hizo, hayatakubaliwa kuhusika katika ujenzi mpya wa Irak.

Msomaji wa serikali ya ujerumani Bela Anda, amesema kwamba ikiwa kweli taarifa kuhusu uamuzi huo wa Marekani ni kweli, basi litakua ni jambo lisiloweza kukubalika. Akasema jambo hilo litakua ni kinyume kabisa na hali ya uhusiano iliyoafikiwa baina ya Marekani na Ujerumani, ambapo nchi hizo mbili zilikubaliana kusahau yaliyopita, na kuendeleza ushirikiano kwa ajili ya siku zijazo.

Msemaji wa serikali ya ufaransa Hervé Ladsous, yeye amesema nchi yake inajadili uhalali wa uamuzi wa serikali ya Marekani.

Nae Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Igor Ivanov, ambae leo hii yuko mjini Berlin, amesema yeyote anayetaka kushiriki katika ujenzi mpya wa Irak, ana haki ya kufanya hivo.

Waraka uliotangazwa na vyombo vya habari leo asubuhi kuwa ni wa wizara ya ulinzi ya Marekani pentagon, unasema makampuni ya Ujerumani, Ufaransa, urusi na Kanada, pamoja na nchi nyingine zilizokataa kujiunga na kampeni ya Marekani nchini Irak, hayakubaliwi kuhusika na ujenzi mpya wa nchi hiyo.