BERLIN :Waziri atetea kubinafsisha nusu ya shirika la reli
21 Septemba 2007Matangazo
Waziri wa uchukuzi wa Ujerumani Wolfgang Tiefensee ametetea mipango yake kuuza asilimia 49 ya shirika la reli linalomilikiwa na taifa la Deutsche Bahn wakati wa mjadala katika bunge la Ujerumani.
Amesisitiza kwamba kubinafisha nusu ya shirika hilo kutaifanya kampuni hiyo kumudu zaidi ushindani wa kimataifa na ameahidi huduma za reli zitaboreshwa.
Mjadala huo unakuja siku moja baada ya kusambaratika kwa mazungumzo kati ya chama cha wafanyakazi madereva wa shirika hilo la GDL na waajiri.
Chama hicho cha wafanyakazi kimekuwa kikishinikiza ongezeko la mshahara la asilimia 31 ambapo Deutsche Bahn imeeleza kuwa ni dhihaka.