1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri mkuu wa Italy, Silvio Berlusconi amezuru Berlin ili kuujadili

8 Desemba 2003
muswada wa katiba ya Muungano wa Ulaya. Baada ya kukutana na Berlusconi, Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder alitamka hawatabadili ibara yo yote muhimu ndani ya muswada huo. Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanategemewa kukutana Ijumaa kuzungumzia katiba. Inafahamika Ujerumani na Italy zinaunga mkono mfumo wa WINGI MARA MBILI wa dola kwa kuambatana na asilimia 60 ya wakaazi. Lakini wanachama wengine, kama Hispania na Poland itakayokuwa mwanachama, inafahamika zinapinga mfumo huo kwa kuhofia zitapoteza sindikizo la kisiasa.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW