1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Ufaransa asisitiza ushirikiano na Ujerumani katika umoja wa Ulaya.

10 Juni 2005

Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Ufaransa ametembelea Ujerumani kujadili mzozo juu ya katiba ya umoja wa Ulaya.

Baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Ujerumani Joschka Fischer, Philippe Douste – Blazy amesema kuwa Ufaransa na Ujerumani zitabaki kuwa nguvu kuu inayoendesha umoja wa Ulaya lakini nchi hizo mbili zinahitaji ushirikiano zaidi na mataifa mengine wanachama wa umoja huo.

Hii ni ziara ya kwanza ya waziri huyo mpya wa Ufaransa nje ya nchi tangu alipotwaa madaraka hayo baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri wiki iliyopita kufuatia kukataliwa kwa katiba ya Ulaya na wapigakura wa Ufaransa katika kura ya maoni.

Douste-Blazy amesema kuwa atatoa maelezo zaidi juu ya vipi Ufaransa na Ujerumani zinaweza kufanyakazi kwa pamoja baada ya mkutano wa umoja wa Ulaya mjini Brussels hapo Juni 16 – 17.