1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Waziri mpya wa Ufaransa atarajiwa mjini Berlin

9 Juni 2005

Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Philippe Douste-Blazy, leo anakuja mjini Berlin, hapa Ujerumani, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika nchi ya nje. Katika tangazo la wizara ya mambo ya kigeni huko Paris ni kwamba kutokana na ziara hiyo anataka kudhihirisha kwamba uhusiano baina ya Ujerumani na Ufaransa ni wa aina maalum. Pia waziri mpya wa Ufaransa juu ya masuala ya Ulaya, Catherine Colonna, anatarajiwa mjini Berlin. Mada za mazungumzo yake ni hali ya baadae ya katiba ya Ulaya baada ya kukataliwa na Wafaransa na Waholanzi katika kura ya maoni, na pia mpango wa matumizi ya fedha kwa Jumuiya ya Ulaya hadi mwaka 2013.

Waziri mkuu wa Uengereza, Tony Blair, jana alisisitiza kwamba nchi yake inataka ipunguziwe mchango wake wa fedha inaoulipa kwa Jumuiya. Alisema mjini London kwamba katika suala hilo hatoregeza kamba. Kutoka mwaka 1984, Uengereza kila mwaka imekuwa ikipunguziwa Euro bilioni 4.6 katika michango yake. Nchi zote 24 zilizobaki ndani ya Jumuiya zinataka iondoshwe afuweni hiyo inayopewa Uengereza.