1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Ziara ya rais wa Korea Kusini nchini Ujerumani.

11 Aprili 2005

Rais wa Korea Kusini, Roh Moo Hyun, amewasili nchini Ujerumani kwa ziara rasmi ya siku tano. Anatarajiwa kuwa na mazungumzo na rais wa Ujerumani, Horst Koehler na kansela Gerhard Schroeder kuhusu uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili. Mazungumzo hayo pia yanatarajiwa kutuwama juu ya Korea Kazkazini na Irak. Rais Hyun anataka kujifunza kutokana na kuungana kwa taifa la Ujerumani na kuuendeleza ule unaoitwa mwaka wa Korea 2005.