BERLIN:Al Gore ataka mkutano ufanyike kujadili hali ya hewa
24 Oktoba 2007Matangazo
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel bwana Al Gore amewataka viongozi waitishe kikao cha dharura kwenye Umoja wa Mataifa mapema mwaka ujao, ili kujadili njia za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza kwenye mkutano juu ya hali ya hewa mjini Berlin,bwana Al Gore, aliekuwa makamu wa rais nchini Marekani amesema kikao hicho kitapaswa kutathmini maazimio yaliyopitishwa kwenye mkutano wa mjini Bali mwezi desemba juu ya kuweka msingi wa makubaliano yatakayochukua nafasi ya rasimu ya Kyoto.
Bwana AlGore ametoa pendekezo juu ya viongozi hao kukutana kila baada ya miezi mitatu hadi mkataba mpya utakapofikiwa mwaka alfu 2 na kumi, miaka miwili kabla ya rasimu ya Kyoto kufikia mwisho.