1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Bibi Markel ana matumaini ya kuundwa serikali ya CDU na SPD

29 Septemba 2005

Kiongozi wa chama cha wahafidhina Christian Democrats-CDU nchini Ujerumani Bibi Angela Merkel, amesema kwamba muungano wa vyama vikubwa kati ya chama chake na Social Democrats-SPD cha Kansela Gerhrad Schroeder , ndiyo uwezekano mkubwa uliopo kwa wakati huu. Bibi Merkel alitoa matamshi hayo baada ya mkutano na Viongozi wa chama cha Kiliberal Free Democrats-FDP, ambacho CDU ilikipendelea kuwa mshirika wake pindi ungepatikana wingi wa kutosha kuweza kuunda serikali, baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Septemba 18. SPD na CDU vilikua na mazungumzo jana, lakini bado havikuweza kukaribiana juu ya suala la nani aiongoze serikali ya mseto ya vyama hivyo vikubwa, kama Kansela.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW