1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Bunge lapitisha bajeti ya 2004

28 Novemba 2003

Baraza la chini la bunge la Ujerumani
limepitisha bajeti ya mwaka 2004 kufuatia
mjadala mzito.
Chama cha upinzani cha Christian
Demokrat na kile cha Free Demokrat vilijaribu
kukwamisha muswada huo kwa kumshutumu Waziri
wa Fedha wa Ujerumani Hans Eichel kwa
kuwasilisha bajeti inayokiuka katiba.Vimesema
kwamba matumizi yake ni makubwa mno kuliko
uwekezaji wake.Akijibu shutuma hizo Eichel
amesema madeni mapya ni kitu cha ulazima
kuinuwa uchumi.Madeni yatagharimia kama
asilimia 10 ya bajeti hiyo ya zaidi ya Euro
bilioni 250.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW