1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Juhudi za kidiplomasia kuutuliza mzozo wa vita vya Lebanon.

23 Julai 2006

Wakati vita vya Libanon vinaendelea, sambamba zinafanywa juhudi zaidi za kuutuliza mzozo huo kwa njia za kibalozi. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Fran-Walter Steinmeier, amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel, Amir Perez. Baadae yatafuata mazungumzo baina yake na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, na pia rais wa Wapalastina, Mahmud Abbas.

Alipokuweko kabla katika mji mkuu wa Misri, Kairo, ambako alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Ahmed Abul Gheit, waziri huyo wa Ujerumani alisema makundi ya kigaidi yasiruhusiwe kuamua ajenda ya Mashariki ya Kati. Lakini alisisitiza kwamba Ujerumani haitaki kuwa mpatanishi katika mzozo huo. Alisema

Peke yake maombi hayasaidii sana. Lazima kuweko masharti ya silaha kusitishwa.

Pia waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice, anatazamiwa kuwasili katika eneo hilo la mzozo. Bado kuna mabishano kuhusu takwa kwamba mapigano hayo yasitishwe. Wakati Marekani na Ujerumani zinaona kwamba kuchukua msimamo mkali dhidi ya Chama cha Hizbullah kuwa ni shuruti ya kusitishwa mapigano hayo, Ufaransa na nchi za Kiarabu zinataka mapigano hayo yasimamishwe mara moja. Kwa mujibu wa gazeti la Israel la HAARETZ ni kwamba Marekani itakubali Israel iendelee kuishambulia Libanon kwa angalau wiki moja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW