1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Schroeder kusimamia zoezi la kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko.

24 Agosti 2005

Kansela wa Ujerumani,Gerhard Schroeder ameahidi kuendesha zoezi la kuhamasisha misaada kwa watu walioathirika na mafuriko katika eneo la kusini mwa Ujerumani.

Kuongezeka kwa kina cha maji,kumewalazimisha askari polisi kuwahamisha watu kutoka katika miji kadhaa ya kusini mwa Bavaria,huku njia za reli zikiwa zimefunikwa na maji na barabara kuu zimefungwa.

Hata hivyo mafuriko yameanza kupungua kidogo leo hii,lakini mamlaka zinazohusika zinaangalia kwa makini uongezekaji zaidi wa kiwango cha maji katika michirizi inayoelekea mito ya Danube,Isar na Inn.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW