1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Kansela wa Ujerumani na kiongozi wa SPD washindwa kuafikiana juu ya mpango wa bima ya afya

22 Septemba 2006

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na kiongozi wa chama cha SPD Kurt Beck wameshindwa kuafikia makubaliano juu kutatua mzozo wa mageuzi katika sekta ya afya.

Wamewaambia waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano wao kwamba wana matumaini makubwa ya kupata ufumbuzi wa mzozo huo katika mkutano wao utakaofuata.

Chama cha Christian Demokrats kinacho ongozwa na bibi Angela Merkel na chama cha Social Demokrats vyote vilipendekeza mifumo tafauti katika mpango wa bima ya afya kwa taifa mnamo mwezi julai lakini pande hizo mbili zimeshindwa kuafikiana juu ya utekelezaji wa mageuzi hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW