BERLIN:Kapuni ya Telecom na mkakati mpya juu ya kazi
1 Machi 2007Matangazo
Zaidi ya wafanyikazi 10,000 wa kampuni kubwa ya simu nchini Ujerumani Deutche Telecom wameandamana kwenye ofisi za kampuni hiyo kupinga mkakati mpya unaojadiliwa ambao utasababisha kuandikwa upya kwa mikataba ya kiasi wafanyikazi 50 elfu.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Telekom Rene Obermann anatarajiwa kutoa maelezo zaidi juu ya mkakati huo kwenye mkutano na waandishi wa habari hii leo.Hata hivyo duru zinasema mabadiliko muhimu yatakuwa ni kubadilishwa kwa saa za kufanya kazi ambapo wafanyikazi itawabidi kufanya kazi kwa muda mrefu.
Chama cha wafanyikazi Verdi kimeonya kwenye maandamano kwamba itapinga mkakati huo wa mageuzi na kwamba wanachama wake katika halmashauri ya Telekom watapinga hatua hiyo.