1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Matamshi ya Schröder yazusha ubishi

15 Juni 2005

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani ametoa wito wa kulegezwa kwa sheria za nchi ili taaluma ya kutengeneza viini tete kwa ajili ya utafiti wa kisayansi iwe huru kuendesha mradi huo kwa mujibu wa sheria za shirikisho la Ujerumani.

Akizungumza katika chuo kikuu cha Göttingen, kansela Gerhard Schröder alisema kutokana na vizuizi vya kisheria Ujerumani inabaki nyuma katika nyanja za teknologia ya elimu ya viumbe na ufundi wa nasaba.

Matamshi hayo ya kansela Schröder yamekosolewa na vyama vya upinzani na hata katika muungano wa vyama tawala vya SDP na chama cha kijani.

Kwengineko raia watatu wa Iraq wanaoishi hapa Ujerumani wamekamatwa kwa tuhuma za kufadhili kikundi cha kigaidi na kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la waasi wa Kikurdi linalo endesha shughuli zake kaskazini mwa Iraq.

Mawakili wa serikali wamesema kuwa watu hao wanashukiwa kuwafadhili wafuasi wa kundi la Ansar al Islam linalo aminika kushirikiana na Abu Musab al Zarqawi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW