1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ndege ndogo yaanguka karibu na ofisi ya Kansela Schroeder

23 Julai 2005

Ndege ndogo imeanguka katikati ya majengo ya bunge na ofisi ya kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani mjini Berlin.

Rubani wa ndege huyo amekufa lakini haikuweza kubainika mara moja juu ya rubani huyo na chanzo cha ajali hiyo pia hakijajulikana hadi sasa.

Hata hivyo waziri wa ndani mjini Berlin Ehrhart Koerting amesema tukio hilo halikuwa jaribio la ugaidi lakini huenda lilikuwa ni ajali au jaribio la kujiuwa.

Polisi wanachunguza vipi ndege hiyo iliweza kufika karibu mno na majengo muhimu ya serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW