BERLIN:Pendekezo la Kansela Schroeder lakubalika
23 Mei 2005Matangazo
Wafanyibiashara mbalimbali na viongozi wa vyama vya wafanyibiashara wamelikubali pendekezo la Kansela Schroeder la kutaka kufanyike uchaguzi wa mapema.
Ludwig Goerge Braun,rais wa chama cha mabaraza ya viwanda na biashara amesema nchi hii haiwezi kuwekwa katika hali ya wasiwasi hadi mwakani. huku mwenyekiti wa chama cha migodi, kemikali na nishati bwana Hubertus Schmoldt akisema huu ni wakati kwa wajerumani wenyewe kuamua ni njia gani watakayoichukua. Juu ya hilo amewataka wajerumani kuamua kati ya uchumi wenye malengo ya kijamii au uchumi wa kibepari.