BERLIN:Schroeder kukutana na Bush Marekani
5 Januari 2004Matangazo
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani anatarajiwa kukutana na Rais George W Bush wakati atakapokwenda nchini Marekani mwezi ujao baada ya hitilafu juu ya suala la Iraq kudhoofisha uhusiano kati ya Marekani na Ujerumani.
Msemaji wa Schroeder amesema Kansela atakuwepo nchini Marekani hapo tarehe 26 na 27 mwezi wa Februari na atafunguwa maonyesho ya sanaa ya Baroque kutoka mji wa mashariki wa Ujerumani wa Dresden huko Jackson Mississipi ambapo Bush pia amealikwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa msemaji huyo inaweza kuhesabiwa kuwa kutakuwepo na mkutano lakini itategemea Rais wa Marekani kuamuwa aidha mkutano huo ufanyike Jackson au Washington.
Hatua ya Schroeder ya kupinga vikali vita viliyvoongozwa na Marekani dhidi ya Iraq imedhoofisha vibaya uhusiano kati ya serikali ya Berlin na Washington lakini Ujerumani imekuwa mbioni kurekebisha uhusiano huo na mshirika wake mkubwa wa pili wa biashara baada ya Ufaransa.
Ujerumani ilikubali mwezi uliopita kutowa msamaha mkubwa wa madeni kwa Iraq licha ya Marekani kuwaaudhi wapinzani wa vita vya Iraq kwa kusema kwamba itawazuwiya wasipatiwe kandarasi za kuijenga upya nchi hiyo.