BERLIN:Ujerumani kuongeza msada wa fedha kwa Afghanistan
6 Novemba 2007Matangazo
Ujerumani imesema kuwa itaongeza msaada wa fedha kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa Afghanitan.
Balozi wa Ujeurmani katika umoja wa mataifa Thomas Matussek ameeleza hayo mbele ya ukumbi wa baraza kuu la umoja wa mataifa kwamba Ujerumani itazingatia kuiunga mkono Afghanistan hadi malengo yaliyotarajiwa ya kupatikana taifa lenye utulivu yatakapokamilika.
Bwana Matussek amesema kwamba Ujerumani imeongeza misaada ya kifedha kufikia Euro milioni 90 mwaka huu na inapanga kuongeza kiwango hicho hadi kufikia Euro milioni 110 katika mwaka ujao wa 2008.