BERLIN:Ujerumani na Japan zataka vikwazo vya silaha dhidi ya China viendelee
11 Januari 2007Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wamesema kuwa vikwazo vya silaha vilivyopo hivi sasa dhidi ya China ni lazima viendelee.
Wakizungumza baada ya mkutano wao mjini Berlin, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kuwa Japan inaogopa nguvu za kijeshi za China zinaweza kubadilisha uiwano wa nguvu katika eneo la Asia.
Kwa upande wake Kansela Merkel amesema kuwa serikali yake haina nia ya kujiondoa katika vikwazo hivyo.
China Iliwekewa vikwazo vya silaha mnamo mwaka 1998 kufuatia mauaji ya wanafunzi waliyokuwa wakiandamana kudai demokrasia nchini humo.
Waziri Mkuu huyo wa Japan anaendelea na ziara yake ya Ulaya, ambapo leo hii atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Japan kutembelea Makao Makuu ya Umoja wa Kujihami wa Ulaya NATO mjini Brussels Ubelgiji.