1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Ujerumani yapinga kushiriki katika jeshi la kulinda amani Lebanon.

24 Julai 2006

Serikali ya Ujerumani bado ipo katika uangalifu kuhusu uwezekano wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Ulaya huko Mashariki ya kati.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Gernot Erler amesema, jeshi kama hilo la kulinda amani ni sehemu ya Umoja wa Mataifa kwa makubaliano na pande mbili ya Israel na Lebanon.

Mapema Ujerumani haijatamka rasmi kama vikosi vyake vitashiriki katika jeshi la kulinda amani linaloundwa na Umoja wa Nchi za Ulaya kwenda huko kusini mwa Lebanon.

Huko Berlin chama cha upinzani cha mrengo wa kushoto kimekataa ushiriki wowote wa wanajeshi wa Ujerumani katika mpango huo wa jeshi la kulinda amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW