1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Vikosi vya majini vya Ujerumani vya jiandaa kuelekea Lebanon.

21 Septemba 2006

Kundi la kwanza la jeshi la wanamaji la Ujerumani linajitayarisha kuelekea katika fukwe za Lebanon, siku moja baada ya wabunge kutoa idhini mpango huo.

Ujerumani napanga kutuma hadi wanajeshi 2,400 kama sehemu ya kikosi cha wanamaji kitakachopiga doria katika fukwe za Lebanon kuzuia meli zinazosafirisha silaha za wanamgambo wa Hezbollah kinyume na sheria.

Jumla ya Manuwari nane zikiwemombili za kivita, na nne kupiga zinatarajiwa kuwasili katika mwambao wa Lebanon wiki mbili kutoka sasa.

Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Ujerumani Bundesvea kupelekwa katika eneo la Mashariki ya kati.

Jana Bunge la Ujerumani Bundestag limepiga kura kwa wingi mkubwa kuunga mkono kujiunga wanajeshi wa Ujerumani na vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani nchini Lebanon.

Vikosi vya Ujerumani vitasalia hadi Agosti mwakani Kansela Angela Merkel amesema shughuli za vikosi hivyo vina umuhimu wa kihistoria.

Aidha amekiri kwamba gharama za ulinzi namna zilivyo hivi sasa haziruhusu kugharamia shughuli nyengine za kulinda amani ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW