1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Vyama ndugu CDU/CSU vyamchagua Merkel kubakia kiongozi wao bungeni

21 Septemba 2005

Vyama vya kihafidhina nchini Ujerumani vimemthibitisha mgombea wake wa ukansela Angela Merkel kuwa kiongozi wao bungeni.

Zaidi ya 98 asilimia ya wabunge kutoka vyama ndugu vya Christian Demokrats CDU na CSU wamempigia kura Merkel kubakia kwenye wadhifa huo.

Merkel aliitisha kura hiyo miongoni mwa washirika wake wa kihafidhina baada ya chama chake kushindwa kupata wingi mkubwa katika uchaguzi wa serikali.

Waziri wa mambo ya nje Joschka Fischer kutoka chama cha FDP amesema anaamini kwamba chama chake kitakuwa kwenye upinzani na hivyo haoni haja ya kubakia kwenye wadhifa wa uongozi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW