1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Ujerumani hausiki na mpango wa silaha kwa Saudia.

4 Agosti 2005

Kansela wa zamani wa Ujerumani,Helmut Kohl ametoa ushahidi wake mahakamani akimsafisha aliyekuwa waziri katika serikali yake anayekabiliwa na kesi ya rushwa, hakuhusika na mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia mwaka 1991.

Holger Pfahls,aliyewahi kuwa naibu waziri wa ulinzi katika serikali ya Bwana Kolh wakati huo,alikiri kukubali kupewa kiasi cha euro karibu milioni mbili na kuidhamini Saudi Arabia ipatiwe silaha wakati wa vita vya kwanza vya Ghuba.

Hata hivyo waendesha mashtaka wameliondoa shitaka la rushwa linalomkabili Pfahls,baada ya Bwana Kohl kueleza kuwa yeye mwenyewe ndie aliyeidhinisha mpango huo,ikiwa ni sehemu ya makubaliano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Bwana Kohl amesema aliamua kutolewa haraka kwa magari kutoka katika jeshi la Ujerumani baada ya kukataa maombi ya kupeleka wanajeshi wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW