Berlusconi afutiwa mashitaka ya ufisadi
15 Februari 2023Matangazo
Mahakama mjini Milan imefanya uamuzi kuwa Berlusconi mwenye umri wa miaka 86 na washitakiwa wengine 28 wengi wao wanawake hawana hatia.
Berlusconi akanusha kula njama kumuangusha Draghi
Waendesha mashitaka walisema Berlusconi aliwalipa wanawake hao kutoa ushahidi wa uwongo katika kesi mbili za kwanza, wakati alituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kukuza ukahaba wa wasichana wadogo.
Berlusconi ambaye ni mfanyabiashara na mbunge, amefutiwa mashitaka kwa kukosekana ushahidi.