1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLUSCONI ANAWEZA KUSHTAKIWA:

14 Januari 2004

ROMA: Mahakama ya Katiba nchini Itali imebatilisha sheria iliompa waziri mkuu wa Itali Silvio Berlusconi kinga ya kutoshtakiwa wakati wa kuwepo madarakani.Uamuzi huo sasa unafungua njia ya kuendelea na kesi ya rushwa dhidi ya Berlusconi.Kesi hiyo ilisimamishwa baada ya bunge la Itali kupitisha sheria ya kumpa kinga Berlusconi na maafisa wengine 4 wa ngazi za juu ikiwa ni pamoja na rais wa nchi.Katika kipindi cha miaka kumi ya nyuma,bilionea Berlusconi-mwana biashara aliekuja kuwa mwanasiasa baadae amefikishwa mahakamani mara nane kwa mashtaka mbali mbali ya honga kuhusika na milki yake ya kibiashara.Berlusconi ni tajiri anaedhibiti vyombo mbali mbali vya habari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW