1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERNE: Waswissi waunga mkono sheria kali za uhamiaji

24 Septemba 2006

Matokeo ya mwanzo ya kura ya maoni iliyopigwa nchini Uswissi leo hii huonyesha kuwa zaidi ya asili mia 70 ya Waswissi wameunga mkono kupitisha sheria kali zaidi kuhusu maombi ya hifadhi ya kisiasa.Kuambatana na sheria hizo mpya itakuwa vigumu zaidi kwa wakimbizi kupata misaada ya kijamii na itakuwa rahisi kwa maafisa wa nchi hiyo kuwafukuza waomba hifadhi ya kisiasa wasiokuwa na vyeti vya utambulisho.Watu wasio na mafunzo ya kazi kutoka nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya,hawatoruhusiwa kuingia Uswissi.Wageni vile vile watapaswa kujijumuisha zaidi katika jamii ya Kiswissi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW