1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Beyonce ampigia debe Harris huko Texas

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Hatua hiyo sio kwa ajili ya kutumbuiza lakini kujitokeza hadharani kumuunga mkono mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Democratic.

Beyoncé alimkumbatia makamu huyo wa rais kwa muda mrefu kabla ya kuondoka
Beyoncé alimkumbatia makamu huyo wa rais kwa muda mrefu kabla ya kuondokaPicha: Annie Mulligan/AP/dpa/picture alliance

Badala ya kuimba, Beyoncé alihutubia umati kwa dakika kadhaa, akisema hakuwepo hapo kama mtu mashuhuri au mwanasiasa, lakini kama mama. Beyoncé awaomba Wamarekani kumuunga mkono Kamala Harris haswa kuhusu sera zake za utoaji mimba.

Wagombea wa urais wa Marekani Kamala Harris na Donald Trump wamezidisha kampeni zao huku ikisalia siku kumi kabla ya uchaguzi. Kwa upande wake Trump amepewa ungwaji mkono mkubwa wa bilionea Elon Musk.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW