1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Biashara Uganda zaathirika na maandamano ya Kenya

28 Juni 2024

Biashara nyingi Uganda zinaelezewa kupata hasara kubwa kutokana na hali ya maandamano katika nchi jirani ya Kenya. Shughuli za usafirishaji mizigo kutoka au kuelekea Bandari ya Mombasa zimedorora.

Uganda | Wafanyabiashara
Wafanyabiashara wa UgandaPicha: Hajarah Nalwadda/Xinhua/picture alliance

Kuna msemo kwamba Kenya ikipiga chafya Uganda hupata mafua. Hii ni kutokana na utegemazi mkubwa wa Uganda kwa Kenya kama njia ya kuingiza au kuuza bidhaa za biashara na vitu vingine vingi. Asli mia 80 ya bidhaa za Ugnda hupitia Kenya.Kufutia ghasia za maandamano ambazo zimekumba Kenya wiki hii, athari zake zimenza kuhisika Uganda.

Kulingana na shirikisho la wenye viwanda Uganda, kila siku wanachama wake kwa jumla wamepata hasara ya kati ya dola milioni 10 na 13 kufuatia mashaka ya mazingira ya kibiashara kati ya nchi hizo.Kenya na Uganda kujenga njia ya reli

Biashara ya mitumba UgandaPicha: Badru Katumba/AFP

Hii ina maana kuwa biashara ya bidhaa za Uganda ambazo zingeuzwa au kupitia Kenya na pia zile zinazoagizwa kutoka Kenya zimekumbwa na tatizo kubwa la mashaka ya uchukuzi wafanyabiashara wakisitisha mipango yao kwa kuhofia kupata hasara. Mkurugenzi wa shirikisho la wenyeviwanda Uganda ambaye pia ni mtaalama wa sera za uchumi Allan Senyondwa amesema.

"Hasara kwa wastani ni kwa bidhaa za kuuzwa nje ni dola milioni tatu na kwa zile zinazoingizwa ni dola milioni 8 kwa siku na la muhimu ni kuona kwamba kuna tahadhari hasara isiongezeke."

Kwa upande wa usafiri, kati ya mabasi 20 ambayo hufanya safari  kati ya miji mikuu ya Kampala na Nairobi, ni mabasi nane tu yamendelea na shughuli za kusafirisha abiria huku baadhi yake yakielezewa kuwashusha abiria miji inayokaribia Nairobi.Maandamano Kenya, watu 7 wakimbizwa hospitalini

Kisa cha basi moja lilikuwa likija Uganda kuvamiwa na kundi fulani na watu na mizigo yao kuporwa ndicho kilileta usiki wa kuamkia jumatano ndicho kilizidisha wasiwasi miongoni mwa makampuni. Ni kwa ajili hii ndipo watu wanaotaka kusafiri wameshauriwa kufanya hivyo nyakati za mchana hadi wakati hali itakaporejea shwari. Haya hapa maoni ya watu mbalimbali.

Wafanyabiashara wakiuza mitumba soko la Owino KampalaPicha: Badru Katumba/AFP

Kulingana na wadau katika sekta binafsi ,si tu sekta ya biashara imeathirika lakini pia utalii. Mataifa ya Kenya Uganda na Rwanda yana mpango ambapo mtalii akipewa kibali cha visa na mojawapo ya nchi hizo, ana fursa kutembelea zingine kati ya hizo.

Kenya yaimarisha usalama ikihofia maandamano mapyaKwa hiyo watalii ambao walikuwa na mpango wa kuja afrika mashariki wakinufaika kutokana na mpango huo yamkini wameahirisha safari zao. Allan Senyondwa ametoa mtazamo huu.

"Kwa kuwa rais wa Kenya ameitikia mwito wa vijana basi vijana hawana sababu kuendelea na maandamano kwani na tutarajie kuwa hali itarejea kuwa ya kawaida haraka iwezekanavyo".

Hata hivyo kuna matumaini kwamba kufuatia tamko la rais wa Kenya kutupilia mbali muswaada wa kifedha iliosababisha ghasia hizo, haitachukua muda mrefu hali kurejea kuwa ya kawaida.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW