1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

'Mapinduzi ya kijani'

Kalyango, Siraj21 Februari 2008

Kumependekezwa 'mapinduzi ya kijani'

Ramani ýa UgandaPicha: AP

Mashirika makubwa ya kimataifa kama vile ya Rockefeller na wakfu wa Bill Gates yanafanya mikakati ya kuwekeza barani Afrika katika sekta ya kilimo.Lengo likiwa kupata soko sio tu kwa chakula chao lakini pia kwa kwa mbegu zao .Mmoja wa mataifa ya kiafrika ambayo yanaonekana yamelengwa na mipango hiyo ni Uganda.


Washirika wakuu wa kibiashara wa Uganda,sio tu wanatafuta masoko ya chakula lakini pia wanataka masoko ya mbegu.


Hii inatokea katika msukumo uliopewa jina la 'mapinduzi mapya ya kijani'.Msukumo huo unayahusisha mashirika ambayo yanahusika na kemikali.


Mashrika hayo yanapigwa jeki na mashirika ya huduma za kiutu-,mkiwemo wakfu wa Rockefeller na wakfu wa Bill na Melinda Gates.


Shirika lingine linalosaidia kampeini hiyo ni la wakfu wa Yara-lililoanzishwa na Yara International mwaka wa 2005.Yara ni maarufu duniani kuwa mstari wa mbele kutengeneza pembejeo.


Kampuni hii yenye makao yake makuu nchini Norway,ndio kampuni pekee ya kimataifa inayotengeneza pembejeo ambayo imetia mizizi barani Afrika kwa kipindi cha miaka 25 iliopita.


Shirika linalotoa misaada la Marekani-USAID- nalo pia halijabaki nyuma katika mchakamchaka huu.Pia linafadhili miradi kadhaa ya kuzalisha mbegu kwenye maabara barani Afrika,sanasana kugharimia taasisi kadhaa za serikali zinazohusika na utafiti wa kilimo.

Shirika hilo lina ushawishi mkubwa kuhusu kazi na ajenda ya taasisi hizo kama ilivyo nchini Uganda.

Wahisani hawajaisha,kwani serikali ya Ujerumani nayo inahusika moja kwa moja.


Na shirika lingine muhumu linalojihusisha pia ni Benki ya Dunia.

Imechangia sana katika kukuza sera ya ulegezaji masharti tangu mwaka wa 1980. Hatua hiyo imesababisha mataifa mengi ya kiafrika kuweka wazi masuala ya kilimo.


Ushauri wake umechangia soko la mbegu barani Afrika, kuwa wazi kutoka mikono ya serikali, na hilo kusaidia kutayarisha kujihusisha kwa makampuni ya kibinafsi.


Shirika la biashara ya mbegu la Marekani-ASTA liliunda kitengo cha Afrika-kwa kifupi-AFSTA-kama chombo cha kukuza sekta ya mbegu katika mataifa kadhaa ya kiafrika.


Kulingana na jarida la kukuza kilimo na maenedeleo ya sehemu za mashambani la Marekani-kitengo cha Afrika cha shirika la biashara ya mbegu la Marekani,kazi kuu ni kukuza pamoja na kuoanisha sera za mbegu kwa upendeleo wa asili mia tano wa mbegu za Marekani kupatiwa soko katika kanda hizo. Soko hilo ni lazima liwe la kipindi cha miaka mitano.


Uganda ni miongoni mwa mataifa hayo yaliyolengwa na mpango huo.

Soko la mbegu zake ni dogo likilinganishwa na la mataifa mengine ya afrika.Kila mwaka gharama ya mauzo yake ya ndani ni dola millioni 6-huo ulikuwa mwaka wa 2005 ikilinganishwa na dola millioni 217 ya Afrika Kusini au dola millioni 50 ya nchi jirani ya Kenya.


Tayari mbegu za Kenya kuuzwa nchini Uganda.


Shirika la utafii wa kilimo la kitaifa NARO limekuwa likitoa aina mpya ya mbegu kwa mradi wa mbegu wa Uganda ili kutayarishwa.

Pia mradi huo wa mbegu wa Uganda ulikuwa na jukumu la kuuza na kusambaza mbegu hizo kwa wakulima.


Hayo yote yalibadilika miaka ya 1990 kutokana na sera ya kulegeza kamba na kujijenga upya.


Sasa mradi huo umesha achwa wazi na soko la mbegu limetoka mikononi mwa serikali.

Kwa sasa kuna kampuni takriban 10 zinazohusika na mbegu nchini Uganda.

Sheria zimebadilishwa ili kuwezesha hali hiyo kutokea.

Walio changia hilo kufikwa ni serikali ambazo zinatoa misaada,mashirika hisani,Benki ya dunia, wanasiasa wa uganda na vigogo mbalimbali.


Magazeti ya Uganda mwaka jana yaliripoti kuwa wakfu za Rockfeller na Gates zimetoa dola millioni 150 kwa Uganda ili kushughulikia kile kilichoitwa mpango wa mapinduzi ya kijani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW