Biashara vijijini Barani Afrika
4 Juni 2007Mashirika makubwa ya kibiashara sasa yameanza kutafuta soko katika maeneo ya watu walala hoi, kuanzia Afrika kusini hadi Brazil.
Hii imefatia soko la mashirika ya kibiashara kupungua katika miji mikuu, kutokana na bidhaa mbali mbali kufurika mijini na hali watu wa vijijini wengi wao hawawezi kumudu bei ya bidhaa za mijini.
Mashirika ya kimataifa ya biashara kwa muda mrefu, yamekua yakipuuza umuhimu wa watu wanaoishi vijijini, wengi wao wakiwa masikini, sasa yamegundua kua watu wenye kipato cha chini nao wanastahiki kua na maisha mazuri alau waweze kupata bidhaa muhimu kwa bei nafuu,mfano mashirika ya biashara ya Danone na Unilever, yameanza kuuza vijijini na pia mijini kwenye masoko ya hadharani, maziwa ya mtindi (maziwa lala) ,Sabuni na kubwa zaidi simu za mkononi, zimekua kivutio kikubwa kwa watu wa vijijini.
Kuna watu billioni 4 masikini Duniani, na 60% ya idadi ya watu duniani, wanaishi kwa chini ya $2 kwa siku, na sasa watu hao ndio wanaolengwa katika kuliinua soko la mashirika ya kibiashara.
Kampuni ya kutengeneza vyakula ya Danone kutokea Ufaransa pamoja na Kampuni itwayo Clover ya Afrika kusini , yenye kutengeneza vyakula vya maziwa, zimeanzisha mradi wa kuuza vipaketi vya maziwa lala, yenye vitamini nyingi kwa Rand 1 sawa na centi 14 za Dollar.
Bi Maria Pretorius meneja wa Masoko anasema vipaketi hivyo vya maziwa vinasambazwa hadi kwenye Mashule ili kuelezea lishe iliomo pia kina Mama wanaopewa kazi hio, huenda nyumba hadi nyumba ,wakiuza bidhaa hizo, na kama bidhaa hizo zingelipitia kwenye maduka makubwa ya Supermaket isingewezekana kuuza kwa Rand moja, alisema Bi Maria Pretorius.
Mama moja aliepewa kazi ya kusambaza bidhaa hizo, Joyce Daka ,anasema kwa siku anaweza kuuza vipaketi vya maziwa ya mtindi au maziwa lala ,zaidi ya700 katika vitongoji vya mji wa Johannesburg, huku kila kipaketi anachouza hupewa faida ya cent 20 za Rand na hali mshahara wake kwa mwezi unafikia Rand 2000 za Afrika kusini sawa na $ 287.
Nchini Kenya nako kulianzishwa Benki ya watu wa kipato cha chini, Equity Bank, na inasemekana imeweza kupata faida kubwa kiasi kwamba mwaka jana Benki hio ilitiwa kwenye shirika la Hisa kuu la Nairobi stock Exchange na pato lilopatikana kwa kila hisa lilikua kubwa mara mbili mwaka jana.
Nayo kampuni ya Unilever inayotengeneza sabuni, shampoo ya kuogea na sabuni nyenginezo imekua na mpango huo huo kuwapa kina mama kazi ya kuuza bidhaa hizo nyumba hadi nyumba nchini Msumbiji,
Sri lanka na Bangladesh na imesaidia sana kina mama wa vijijini kupata kazi ili kuendesha maisha yao.
Barani Afrika mashirika ya biashara yameanza kuweka vituo vya kuuzia Simu za mkononi mashambani , ingawaje imekua ni 15% ya simu zilizoko vijijini lakini idadi hio sasa imeanza kupanda kwa kasi.
Bw C.K Prahalad mshauri wa mambo ya kibiashara, akiwa pia Professor katika chuo kiku cha Michigan nchini Marekani anasema,
kusambazwa kwa simu za mkononi miongoni mwa watu masikini, sio tu kuongeza faida lakini wakulima wa vijijini wameweza kujua bei ya mazao, kwa soko la kimataifa ili kuboresha biashara yao.
Watu hawa billioni 4 ambao wamo kwenye rika la umasikini duniani, sasa wanakadiriwa kununua bidhaa za Dollar Trillioni 5 kwa mwaka .
Hii imefatia soko la mashirika ya kibiashara kupungua katika miji mikuu, kutokana na bidhaa mbali mbali kufurika mijini na hali watu wa vijijini wengi wao hawawezi kumudu bei ya bidhaa za mijini.
Mashirika ya kimataifa ya biashara kwa muda mrefu, yamekua yakipuuza umuhimu wa watu wanaoishi vijijini, wengi wao wakiwa masikini, sasa yamegundua kua watu wenye kipato cha chini nao wanastahiki kua na maisha mazuri alau waweze kupata bidhaa muhimu kwa bei nafuu,mfano mashirika ya biashara ya Danone na Unilever, yameanza kuuza vijijini na pia mijini kwenye masoko ya hadharani, maziwa ya mtindi (maziwa lala) ,Sabuni na kubwa zaidi simu za mkononi, zimekua kivutio kikubwa kwa watu wa vijijini.
Kuna watu billioni 4 masikini Duniani, na 60% ya idadi ya watu duniani, wanaishi kwa chini ya $2 kwa siku, na sasa watu hao ndio wanaolengwa katika kuliinua soko la mashirika ya kibiashara.
Kampuni ya kutengeneza vyakula ya Danone kutokea Ufaransa pamoja na Kampuni itwayo Clover ya Afrika kusini , yenye kutengeneza vyakula vya maziwa, zimeanzisha mradi wa kuuza vipaketi vya maziwa lala, yenye vitamini nyingi kwa Rand 1 sawa na centi 14 za Dollar.
Bi Maria Pretorius meneja wa Masoko anasema vipaketi hivyo vya maziwa vinasambazwa hadi kwenye Mashule ili kuelezea lishe iliomo pia kina Mama wanaopewa kazi hio, huenda nyumba hadi nyumba ,wakiuza bidhaa hizo, na kama bidhaa hizo zingelipitia kwenye maduka makubwa ya Supermaket isingewezekana kuuza kwa Rand moja, alisema Bi Maria Pretorius.
Mama moja aliepewa kazi ya kusambaza bidhaa hizo, Joyce Daka ,anasema kwa siku anaweza kuuza vipaketi vya maziwa ya mtindi au maziwa lala ,zaidi ya700 katika vitongoji vya mji wa Johannesburg, huku kila kipaketi anachouza hupewa faida ya cent 20 za Rand na hali mshahara wake kwa mwezi unafikia Rand 2000 za Afrika kusini sawa na $ 287.
Nchini Kenya nako kulianzishwa Benki ya watu wa kipato cha chini, Equity Bank, na inasemekana imeweza kupata faida kubwa kiasi kwamba mwaka jana Benki hio ilitiwa kwenye shirika la Hisa kuu la Nairobi Stock Exchange na pato lilopatikana kwa kila hisa lilikua kubwa mara mbili mwaka jana.
Nayo kampuni ya Unilever inayotengeneza sabuni, shampoo ya kuogea na sabuni nyenginezo imekua na mpango huo huo kuwapa kina mama kazi ya kuuza bidhaa hizo nyumba hadi nyumba nchini Msumbiji,
Sri lanka na Bangladesh na imesaidia sana kina mama wa vijijini kupata kazi ili kuendesha maisha yao.
Barani Afrika, mashirika ya biashara yameanza kuweka vituo vya kuuzia Simu za mkononi mashambani , ingawaje imekua ni 15% ya simu zilizoko vijijini lakini idadi hio sasa imeanza kupanda kwa kasi.
Bw C.K Prahalad mshauri wa mambo ya kibiashara, akiwa pia Professor katika chuo kiku cha Michigan nchini Marekani anasema,
kusambazwa kwa simu za mkononi miongoni mwa watu masikini, sio tu kuongeza faida lakini wakulima wa vijijini wameweza kujua bei ya mazao, kwa soko la kimataifa ili kuboresha biashara yao.
Watu hawa billioni 4 ambao wamo kwenye rika la umasikini duniani, sasa wanakadiriwa kununua bidhaa za Dollar Trillioni 5 kwa mwaka.