Biashara ya silaha yapungua duniani, yaongezeka Ulaya
13 Machi 2023Taasisi hiyo ya kimataifa hufanya utafiti na kulinganisha biashara ya silaha kwa kipindi cha miaka minne na ni kwasababu biashara ya silaha hubadilika badilika kila mwaka na kwa mtazamo wa taasisi hiyo utafiti wa muda mrefu ni bora zaidi katika kuakisi hali halisi ilivyo.
Pieter Wezeman ni mtafiti katika taasisi ya SIPRI amezungumza na DW na kuyaweka wazi masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye ripoti hiyo.
''Mabadiliko makubwa tuliyoyaona katika jukwaa la biashara ya silaha kimataifa,ikiwemo msaada wa kijeshi ni kwamba kwanza usafirishaji silaha katika nchi za Ulaya umeongezeka lakini pia ni muhimu kusisitiza kwamba dhima ya Marekani kama msafirishaji mkubwa wa silaha kimataifa pia imeongezeka kwa kiwango kikubwa''
Katika miaka ya hivi karibunia kuanzia mwaka 2018 mpaka 2022 biashara ya silaha kimataifa ilipungua kwa kiasi asilimia 5 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2013 mpaka 2017.
Kwa upande mwingine uagizaji silaha katika nchi za Umoja wa Ulaya na hususan kutoka Marekani uliongezeka kwa asilimia 47,na kwa nchi za Umoja huo ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya kujihami NATO manunuzi ya silaha yaliongezeka kwa asilimia 65.
Lakini sababu ya ongezeko hilo barani Ulaya inajulikana na wala sio jambo la kushangaza-ni vita nchini Ukraine.Nchi hiyo hivi sasa imekuwa ni nchi ya tatu katika zile nchi zinazopokea silaha kwa wingi duniani.Japokuwa huko nyuma nchi hiyo haikuwa na dhima yoyote sio kama mpokeaji wala mnunuzi wa silaha.
Ukraine na silaha
Na pia ni kwasababu nchi hiyo iliyokuwa zamani chini ya muungano wa Kisovieti binafsi ikitengeneza silaha na bado ilikuwa na silaha zake za tangu enzi ya kisovieti kwahivyo haikuwa na mahitaji makubwa ya silaha.
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 mpaka 2022 nchi hiyo lakini ilijikuta ikisimama katika nafasi ya 14 na ukitazama mwaka 2022 peke yake nchi hiyo iko katika nafasi ya 3 katika nchi zilizopokea silaha nyingi duniani.
Kimsingi ripoti ya SIPRI inazungumzia kwa ujumla wake suala la biashara ya silaha ambayo pia inayojumuisha msaada wa kijeshi kama ambavyo inashuhudiwa inavyofanyika kwa nchi kama Ukraine.
Usafirishaji silaha duniani waongezeka - SIPRITaasisi hiyo pia inakumbusha kwamba katika biashara ya silaha kwa nchi kama Ukraine kiwango cha mauzo kiko chini.Imetowa mfano kwamba silaha zilizosafirishwa na Marekani nchini Ukraine ndani ya mwaka 2022 mauzo yake hayawezi kulingana ya yale yaliyopatikana katika nchi nyingine nne zilizonunua silaha kutoka Marekani,za Kuwait,Saudi Arabia,Qatar na Japan.
Na hiyo ni kwasababu nchi hizo zimenunua silaha na mifumo ya kisasa kabisa yenye uwezo mkubwa ikiwemo ndege za kivita.Ukraine kwa upande wake bado inaombi la dharura la kupatiwa ndege za kivita lakini mpaka sasa haijapatiwa ndege hizo na nchi za Magharibi.
Orodha ya wasafirishaji wakuwa wa silaha duniani haijabadilika ambapo Marekani inaongoza ikisafirisha asilimia 40 ya silaha duniani ikifuatiwa na Urusi,Ufaransa iko nafasi ya tatu ikifuatiwa na China na kisha Ujerumani.