1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biashara ya silaha za Ujerumani kwa Saudi Arabia Magazetini

Oumilkheir Hamidou
17 Juni 2019

Biashara ya silaha za Ujerumani kwa Saudi Arabia, walinzi wa mazingira die Grüne wawapita wana SPD na shauri la rais wa zamani Joachim Gauck kutowatenga wafuasi wote wa siasa kali za mrengo wa kulia magazetini.

Deutschland Alb-Kaserne Artillerieortungsradar COBRA
Picha: picture-alliance/dpa/S. Gollnow

Tunaanzia na ripoti kuhusu biashara ya silaha za Ujerumani kwa Saudi Arabia. Gazeti la Badische Zeitung linaandika: "Kwa namna hiyo serikali kuu ya Ujerumani inaipa kichwa Saudi Arabia iendelee kufuata njia ya kuchochea  vita. Hali hiyo inazihusu pia nchi nyengine zinazounda ushirika katika vita vya Yemen ambazo pia zinaagizia kwa wingi silaha kutoka Ujerumani, kwa mfano falme za nchi za kiarabu-Emirati. Sawa na Saudi Arabia na wao pia wanapalilia mivutano katika eneo hilo, lengo likiwa kuitenga Iran inayofuata madhehebu ya kishia na kuanzisha enzi za wasunni Mashariki ya kati. Kwa hivyo nchini Yemen sawa na kwengineko watu wataendelea kufa kwasababu ya silaha za Ujerumani."

 

 AfD wasitengwe moja kwa moja anasema Joachim Gauck

Shauri la rais wa zamani Joachim Gauck la kutowatumbukiza chungu kimoja wafuasi wa makundi yote ya  siasa kali za mrengo wa kulia limeibua mjadala humu nchini. Gazeti la "Passauer Neue Presse" linaandika: "Bila ya shaka Gauck alikuwa na dhamii nzuri. Lakini pendekezo lake la kupanua uwanja wa kuvumilia kuelekea mrengo wa kulia halitopokelewa vyema na wahafidhina sugu ambao bado ni sehemu ya wapenda demokrasia. Kinyume chake watakaofaidika ni wale wanaoitia sumu jamii na kutaka milango iwachwe wazi zaidi hadi kufikia wapigakura wanao yajongelea makundi ya wanazi mambo leo. Rais wa zamani wa shirikisho, Joachim Gauck amesahau kwamba majadiliano pamoja na "wahafidhina wema" ndani au pembezoni mwa chama jumla cha AfD ni sehemu ndogo tu. Na hiyo pia n dio sababu kwanini hadi sasa hakuna wabunge wengi wanaounga mkono spika wa bunge achaguliwe kutoka achama cha siasa kalai za mrengo wa kulia cha AfD."

Walinzi wa mazingira die Grüne wanazidi kuwavutia wapigakura

Mada yetu ya mwisho magazetini inawamulika walinzi wa mazingira die Grüne na jinsi wanavyozidi kupata imani ya wapigakura. Gazeti la" Rhein-Zeitung" linaandika:"Husda wanayoomeana wana SPD, matatizo yanayowazonga washirika katika serikali ya muungano wa vyama vikuu na udhaifu wa chama cha kiliberali cha FDP ndio sababu ya walinzi wa mazingira die Grüne kufanikiwa kuwavutia wapiga kura bila ya shida. Hadi wakati huu walinzi wa mazingira walikuwa wakiangaliwa kama ni wenye kujishughulisha na masuala ya mabadiliko ya tabianchi tu. Lakini  hakuna cha bure na wawekezaji wa fuko la mabadiliko ya tabianchi wametangaza mabilioni ya Euro ambazo katika suala la jinsi ya kugharamia, walinzi wa mazingira wanabidu wafafanue.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inalndspresse

Mhariri: Sekione Kitojo

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW