SiasaMarekani
Biden aamua kujibu shambulizi lililotokea Jordan
31 Januari 2024Matangazo
Rais Biden ambaye hakutoa maelezo kuhusu hatua hizo amesisitiza kuwa hataki kuanzisha vita pana katika Mashariki ya Kati.
Huku akikabiliwa na shinikizo katika mwaka wa uchaguzi nchini Marekani, Biden amesema Iran ndiyo inayosambaza silaha kwa watu waliofanya shambulizi hilo hatari kwenye kituo cha kijeshi.
Ikulu ya White House imeonya kuwa huenda kukawa na hatua kadhaa za kulipiza shambulizi hilo la kwanza kali kufanywa dhidi ya wanajeshi wa Marekani katika kanda hiyo tangu kuzuka vita vya Israel na Hamas Oktoba mwaka jana.
Warepublican wamemhimiza Biden ambaye ni Mdemcrat kuiadhibu Iran kwa shambulizi hilo lililotokea karibu na mpaka wa Jordan na Syria, huku baadhi wakimhimiza kufanya mashambulizi ya moja kwa moja kwa Iran yenyewe.