1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aapa kusaidia wanafunzi na madeni ya mkopo

1 Julai 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amesema mamilioni ya raia wa nchi hiyo wameghadhabishwa na uamuzi wa Mahakama ya Juu wa kufuta mpango wa serikali yake wa kuwasamehe wanafunzi madeni ya mkopo wa elimu ya juu.

USA Washington Weißes Haus | Joe Biden, Präsident
Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Kiongozi huyo amesema anafahamu kwamba Wamarekani wamevunjwa moyo na uamuzi huo wa mahakama, lakini ameahidi utawala wake utapambana kupunguza mzigo wa madeni unaowakabili mamilioni ya watu waliokopa kupata elimu ya juu.

Mahakama ya Juu ya Marekani ilitoa uamuzi huo jana ikisema rais Biden hakuwa na mamlaka ya kutangaza msamaha wa madeni ya mikopo ya elimu ya juu. Msahama huo ulilenga kuwapunguzia au kuwafutia kabisa mikopo ya elimu ya juu mamia kwa maelfu ya Wamarekani.

Kutokana na uamuzi wa mahakama, serikali ya Biden imetangaza hatua nyingine za kupunguza mzigo huo ikiwemo kusitisha kwa muda utozaji faini kwa wale wanaochelewa kulipa na kupunguza kiwango cha malipo ya mkopo kwa kila mwezi kutoka asilimia 10 ya kipato hadi asilimia 5 pekee.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW