Biden adai ameghadhabishwa na mashambulizi hospitali Gaza
18 Oktoba 2023Matangazo
Biden ameyasema hayo mara tu baada ya kuwasili nchini Israel na kukutana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, siku ya Jumatano (Oktoba 18).
Rais huyo wa Marekani alisema nchi yake ingeliipa Israel kila kitu inachohitaji kujilinda yenyewe wakati ikiendeleza vita vyake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas, ambalo ameonekana kulituhumu kwa kufanya shambulizi hilo dhidi ya hospitali.
Soma zaidi: Biden kuizuru Israel wakati ikijiandaa kuivamia Gaza
Israel inadai shambulizi hilo limesababishwa na roketi la Palestina lakini Hamas inakanusha madai hayo.
Biden amedai kundi la Hamas ni baya zaidi kuliko kundi linalojiita Dola la Kiislamu kwa kuwaua raia wa Israel katika shambulizi la Oktoba 7.