1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden aelezea wasiwasi kuhusu machafuko ya baada ya uchaguzi

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Rais Joe Biden amesema anaimani kuwa uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani utafanyika kwa haki, lakini ameibua wasiwasi kuhusu machafuko yanayoweza kutokea.

Rais wa Marekani Joe Biden aelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa machafuko baada ya uchaguzi wa Marekani
Rais wa Marekani Joe Biden aelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa machafuko baada ya uchaguzi wa MarekaniPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

 Akizungumza na waandishi habari Ijumaa jioni kwenye Ikulu ya White House,  Biden amesema hafahamu ikiwa uchaguzi wa Novemba utakuwa wa amani.

Biden alionyesha mashaka kuhusiana na upinzani wa chama cha Republican ikiwa utakukubali matokeo ya uchaguzi. Kampeni za uchaguzi zinapozidi kupamba moto, hofu ya kuchochewa machafuko pia imeongezeka. Jaribio la hivi majuzi la kumuua mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump limeibua mijadala zaidi kuhusu hali ya mpasuko wa kisiasa nchini Marekani.

Kushambuliwa kwa Bunge la Marekani na wafuasi wa rais wa zamani Donald Trump kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi wa 2020, kumeongeza wasiwasi miongoni mwa Wamerekani kuhusu uchaguzi ujao.