1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Biden airuhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu

18 Novemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ameiruhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani na kushambulia miundombinu ya kijeshi ndani ya Urusi.

Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) akisalimiana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) akisalimiana na rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Yuri Gripas/UPI Photo/IMAGO

Hayo yamesemwa na afisa wa Marekani  aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, na hivyo kuthibitisha taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani na ambayo inaashiria mabadiliko makubwa ya sera.

Hatua hiyo iliyokuwa ikitakiwa kwa muda mrefu na Kiev, imechukuliwa saa chache baada ya  Urusi kufanya mashambulizi makubwa  yaliyolenga gridi ya umeme ya Ukraine, na pia ni jibu kwa kitendo cha Korea Kaskazini kupeleka wanajeshi Moscow.

Hata hivyo, bado kitendo cha kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House januari mwakani kinaendelea kuzusha hofu kuhusu mustakabali wa uungaji mkono wa Marekani kwa Kyiv.

Urusi yafanya mashambulizi makubwa Ukraine

Vikosi vya zimamoto vikiwa kazini baada ya mashambulizi ya UrusiPicha: Ukrainian Emergency Service via AP/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Urusi imeshambulia nchi yake kwa makombora 120 na ndege 90 zisizo na rubani 90 siku ya Jumapili.

Mashambulizi hayo makubwa yalilenga miundombinu ya nishati ya nchi hiyo. Rais Zelensky amesema vikosi vya ulinzi vya Ukraine vilifaulu kuangusha makombora 140 ya angani lakini kuna uharibifu uliofanyika.

Soma pia: Nchi za G7 zasisitiza kuendelea kuiunga mkono Ukraine

Ameendelea kuwa katika mji wa Mykolaiv, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yamesababisha vifo vya watu wawili. Watu wengine sita wamejeruhiwa, wakiwemo watoto wawili. Mkuu wa kijeshi wa jiji la Kiyv Serhii Popko amesema mashambulizi hayo mapya ya urusi ya ndege zisizo na rubani na makombora yalikuwa ni makubwa zaidi.

(Vyanzo: AP, DPAE, AFP)

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW