1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Biden ayatembelea makaburi ya kijeshi ya Marekani Ufaransa

9 Juni 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amekamilisha ziara yake nchini Ufaransa leo kwa kutoa heshima zake katika makaburi ya kijeshi ya Marekani ambayo Donald Trump alikwepa kuyatembelea wakati akiwa rais.

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakitoa heshima zao walipohudhuria hafla ya uwekaji shada la maua kwenye makaburi ya wanajeshi wa Marekani ya Aisne-Marne huko Belleau, Ufaransa, Juni 9, 2024.
Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakitoa heshima zao walipohudhuria hafla ya uwekaji shada la maua kwenye makaburi ya wanajeshi wa Marekani ya Aisne-Marne huko Belleau, Ufaransa, Juni 9, 2024.Picha: Elizabeth Frantz/REUTERS

Biden anatumai kuwa hatua hiyo ya leo itamuongezea kura katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwezi Septemba.

Kabla ya kurejea Marekani, Biden alitoa heshima kwa wanajeshi waliouawa, katika makaburi ya Kimarekani ya Aisne-Marne, yaliyoko nje ya mji mkuu Paris.

Soma pia: Macron kumpokea Biden katika ziara rasmi mjini Paris 

Aliweka shada la maua kwenye kanisa la makaburi hayo walikozikwa karibu askari 2,200 wa Kimarekani waliopigana katika Vita Vya Kwanza Vikuu vya Dunia.

Ziara ya Biden nchini Ufaransa iliashiria miaka 80 ya kumbukumbu ya D-Day ambayo ni operesheni ya vikosi vya washirika wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia iliyopelekea kuangushwa kwa utawala wa Kinazi nchini Ujerumani.

Aidha Biden alitumia ziara hiyo kusherehekea ushirikiano kati ya Marekani na Ufaransa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW