1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akataa kujitowa kinyang'anyiro cha urais Marekani

4 Julai 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amekataa kujitowa kwenye uchaguzi wa Novemba, wakati kukiwa na shinikizo kumtaka ajitowe kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kushindwa kwenye mdahalo wake na Donald Trump wiki iliyopita.

Uchaguzi wa Marekani 2024 | Mdahalo wa televisheni| Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani kwenye mdahalo wake na Donald Trump.Picha: Gerald Herbert/AP Photo//picture alliance

Msemaji wake, Karine Jean-Pierre, amekanusha kuwa Biden alimuambia mmoja wa washirika wake wa karibu kwamba uwezekano wa yeye kuchaguliwa tena upo hatarini, endapo atashindwa kurejesha imani ya umma kwake baada ya matokeo mabaya ya mdahalo huo.

Biden amedai kuwa kushindwa kwake kwenye mdahalo huo kulitokana na kulemewa na majukumu na kuchoka sana katika siku za karibuni.

Soma zaidi: Biden akabiliwa na shinikizo kuhusu kampeni yake ya kuwania tena urais

Baadhi ya magavana wa chama chake cha Democrat waliokutana hapo jana na Biden, wamesema bado wana imani naye ingawa wamekiri kuwa mdahalo ulikuwa mbaya kwake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW