1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akutana na rais wa Angola, atangaza ziara ya Afrika

1 Desemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Angola Joao Lourenco wamekutana katika ikulu ya White House kujadiliana kuhusiana na masuala ya miundomsingi na usalama wa kikanda.

Rais wa Angola Joao Lourenco na Joe Biden wa Marekani.
Rais wa Angola Joao Lourenco na Joe Biden wa Marekani.Picha: Luis Tato/Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Angola Joao Lourenco wamekutana katika ikulu ya White House kujadiliana kuhusiana na masuala ya miundomsingi na usalama wa kikanda, wakati ambapo Marekani inataka kukabiliana na ushawishi wa China unaoongezeka barani Afrika.

Katika mkutano huo, Biden amezungumzia uekezaji mkubwa wa Marekani katika mradi mkubwa wa reli Afrika uitwao Lobito unaoiunganisha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Zambia na bandari ya Lobito ya Angola.

Soma pia: Kwanini bara la Afrika ni muhimu kimkakati ?

Lourenco kwa upande wake amempongeza Biden kwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani kubadilisha ushirikiano kati ya Marekani na bara la Afrika.

Biden amesema kwamba ataizuru Angola ingawa hakutoa tarehe kamili atakapofanya ziara hiyo. Rais huyo wa Marekani hajaizuru Afrika katika muhula wake wa urais ambao umesalia miezi kadhaa tu. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW