1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akutana na viongozi wa nchi za mashariki mwa NATO

23 Februari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa nchi za upande wa mashariki mwa Ulaya, ambao ni wanachama wa jumuiya ya Kujihami ya Nato.

Warschau NATO-Treffen Bukarest 9
Picha: MANDEL NGAN/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa nchi za upande wa mashariki mwa Ulaya, ambao ni wanachama wa jumuiya ya Kujihami ya Nato.

Kwenye mkutano huo huko Warsaw Poland, Biden amekariri kujitolea kwa nchi yake kuhakikisha usalama wa washirika wake wa mashariki mwa Ulaya na amejadili msaada kwa Ukraine.

Biden alisisitiza kifungu cha 5 cha jumuiya hiyo ambacho kinaelezea mkakati wa pamoja wa ulinzi wa NATO.

Mkutano huo uliwaleta wakuu wa nchi tisa maarufu kama Bucharest Tisa, ambazo ni Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Estonia, Hungary, Latvia, Lithuania, Poland, Romania na Slovakia.

Nchi hizo zimekuwa zikiunga mkono juhudi za misaada ya kijeshi kwa Ukraine, na zimetoa wito wa misaada zaidi kama mifumo ya ulinzi ya angani kwa taifa hilo linalozongwa na vita.

Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda amesema alimtaka Biden kutumia zana za ziada za kijeshi zilizoko katika mataifa ya Baltic.

Biden aliwasili Warsaw Jumatatu jioni baada ya kufanya ziara ya ghafla mjini Kiev Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW