1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akutana na washirika wake wa Japan na Korea Kusini

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa Japan na Korea Kusini kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki APEC nchini Peru.

Mkutano wa APEC| Joe Biden
Picha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa Japan na Korea Kusini kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki APEC nchini Peru.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Biden amesifu ushirikiano kati ya nchi hizo tatu katika kukabiliana na kile alichokiita ushirika hatari na unaovuruga utulivu baina ya Korea Kaskazini na Urusi.

Biden alitumia nafasi hiyo kuwatuliza washirika wake kabla ya Donald Trump kuchukua madaraka na kuonya juu ya mabadiliko makubwa ya kisiasa.

Mkutano wa kilele wa APEC utakuwa moja ya mikutano ya mwisho ya kimataifa ya Biden kabla ya kuondoka madarakani. Baadae leo, Biden, anatazamiwa kukutana ana kwa ana na Rais wa China Xi kwa mara ya kwanza tangu kongamano la APEC la mwaka uliopita.