Biden amkaribisha Trump Ikulu ya White House
14 Novemba 2024Trump na Rais Joe Biden anayemaliza muda wake, ambao ni mahasimu wa muda mrefu wa kisiasa, walijadili mizozo ya Ukraine na Mashariki ya Kati, sambamba na makabidhiano ya amani ya madaraka.
Biden amempongeza Trump kwa ushindi wake, wakati alimpokaribisha katika ofisi ya rais na kusalimiana naye kwa kushikana mkono, akimuahidi mchakato mzuri wa kumkabidhi mamlaka. Miaka minne iliyopita, baada ya kushindwa katika uchaguzi, Trump mwenyewe alikataa kushiriki katika utaratibu huo wa kukabidhi madaraka.
Msemaji wa Ikulu ya White House Karine Jean-Pierre, aliwaeleza waandishi wa habari kwamba viongozi hao wawili wamejadili masuala muhimu kuhusu usalama wa kitaifa na sera za ndani zinazolikabili taifa hilo na ulimwengu. Mazungumzo yao yalidumu kwa muda wa saa mbili.Rais mteule Donald Trump awateua wapambe wake
Naye mshauri wa usalama wa kitaifa Jake Sullivan alisema Biden alitoa msisitizo kwa Trump kwamba ni muhimu kuendeleza uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine dhidi ya Urusi. Kulingana na Sullivan, Biden amesema uungaji mkono kwa Ukraine ni bora kwa usalama wa taifa wa Marekani kwasababu Ulaya imara na thabiti itazuia nchi hiyo kujiingiza katika vita.
Trump ameahidi kumaliza vita vya Urusi na Ukraine kwa haraka bila kusema jinsi gani.Trump aendelea kupanga safu yake ya uongozi kwa kuteua viongozi wapya
Ama kwa upande wake Trump amelieleza gazeti la New York Post kwamba yeye na Biden walizungumza sana kuhusu Mashariki ya Kati wakati wa mazungumzo yao kwani alitaka kufahamu ni wapi wamefikia. "Nilitaka kujua maoni yake kuhusu tulipo, na ameniambia" New York Times imemnukuu Trump.
Ziara ya Trump imefanyika wakati chama cha Republican kikidhibiti mabunge yote mawili ya Baraza la Wawakilishi na Seneti, huku akiendelea kupanga safu yake ya uongozi.Trump afanya uteuzi mpya, Rubio anatazamiwa kuwa waziri wa mambo ya nje
Kabla ya kwenda Ikulu, Trump alipita katika kambi ya pamoja ya Andrews kwa ndege yake mwenyewe, iliyopewa jina la "Trump Force One.
Alisherehekea ushindi wake pamoja na Warepublican wenzake katika Baraza la Wawakilishi, ambao wameendeleza udhibiti wa baraza hilo, wakifikia viti 218 vinavyohitajika, wiki moja baada ya uchaguzi.