1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden amlaumu Trump kwa uvamizi wa Capitol

7 Januari 2022

Rais wa Marekani Joe Biden amesema mtangulizi wake alijaribu kuzuia demokrasia na ukabidhiaji madaraka kwa njia ya amani.

USA Jahrestag des Capitol Riot | Biden
Picha: Michael Reynolds/AP Photo/picture alliance

Kauli ya Biden ilikuwa sehemu ya hotuba yake ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu wafuasi wa Trump walipolivamia majengo ya bunge Capitol Hill.

Biden na makamu wake Kamala Harris walilihutubia taifa lao Alhamisi wakati nchi hiyo ilipoandaa kumbukumbu ya kwanza, mwaka mmoja tangu wafuasi wa rais wa zamani Donald Trump kuyashambulia majengo ya bunge Capitol Hill.

Wabunge wa Marekani pia walishiriki kumbukumbu hizo na kufanya maombi huku wakiwakumbuka waliouawa wakati wa uvamizi huo.

Kufuatia madai ya Trump kwamba uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu, genge la wafuasi wake lilivamia majengo ya Bunge Januari 6 mwaka uliopita kujaribu kuzuia mchakato wa kuidhinisha ushindi wa Biden.

Watu watano waliuawa na Zaidi ya maafisa watano wa polisi walijeruhuiwa wakati w auvamizi huo wa bunge Januari 6, 2021.Picha: Douglas Christian/Zumapress/picture alliance

Akitoa hotuba yake Alhamisi katika eneo ambako vurugu hizo zilitokea, Rais Biden alisema ni sharti Marekani ihakikishe matukio kama hayo hayatokei tena.

Biden asema demokrasia ya Marekani ilishambuliwa.

"Rais wa zamani wa Marekani alieneza uwongo mwingi kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu, rais hakushindwa tu katika uchaguzi lakini alijaribu kuzuia ukabidhiaji madaraka kwa njia ya amani huku genge likishambuliwa Capitol”.

Biden aliwahimiza raia wa Marekani kuhakikisha wanarekebisha uharibifu ambao umefanyiwa demokrasia ya nchi yao.

Trump akataa wito wa kutoa ushahidi bungeni

"Kwa sasa ni lazima tuamue tunataka tuwe nchi ya aina gani. Je tutakuwa nchi ambayo inakubali machafuko ya kisiasa kama jambo la kawaida? Hatuwezi kuruhusu kuwa taifa kama hilo. Suluhisho ni kubaini ukweli na tuuzingatie,” Biden alihimiza.

Wito wa kuondoa migawanyiko ya kisiasa Marekani

Wademokrat wakiwakumbuka watu waliouawa wakati wa uvamizi wa majengo ya bunge nchini Marekani Januari 6, 2021.Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Makamu wake Harris aliyezungumza mwanzo, alisema umoja na demokrasia ya nchi hiyo inajaribiwa na akawahimiza raia kuungana kuilinda demokrasia yao.

Spika wa bunge Nancy Pelosi ambaye ni miongoni mwa vigogo wa chama cha Democratic alisema anatumai watu wataungana ili kusuluhisha migawanyiko ya kisiasa iliyoko.

Trump: Biden 'aigawa Marekani zaidi'

Kufuatia hotuba ya Biden, rais wa zamani Trump alitoa taarifa akimshutumu Biden kwa kile alichokitaja kuwa kujaribu kuigawa Marekani Zaidi.

Licha ya kufutiwa mashitaka,Trump bado aendelea kuandamwa

Trump aliendeleza madai yake yasiyokuwa na uthibitisho kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ulikumbwa na udanganyifu.

Japo wabunge wa pande zote walikuwepo bungeni wakati wa kumbukumbu hizo, warepublican wengi wameendelea kumtetea Trump.

Watu wasiopungua 725 wameshashtakiwa kufuatia vurugu hizo. Aidha Zaidi ya watu 300 wakiwemo wapambe na waliokuwa maafisa wa Trump wameshahojiwa na jopo la bunge linalochunguza tukio hilo.

DW/AFP/AP