1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden ampendekeza Harris baada ya kujiondoa mbioni

22 Julai 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amethibitisha kuwa anajiondoa katika kinyang'anyiro cha uhaguzi wa rais 2024 dhidi ya Donald Trump. Biden amesema anaamini uamuzi huo ni kwa maslahi ya chama chake na nchi.

Uchaguzi wa rais Marekani
Biden ampendekeza makamu wake wa rais Kamala Harris baada ya kujiondoa mbioniPicha: Ricky Fitchett/ZUMA Press Wire/picture alliance

Alimpendekeza makamu wake Kamala Harris kuchukua nafasi yake katika mbio za kuingia Ikulu. Harris katika taarifa aliisifu hatua ya Biden kukataa uteuzi wa chama cha Democratic, akiitia kuwa ya "kizalendo." Aliapa kufanya bidii na kupata uteuzi wa Democratic na kumshinda Trump.

Soma pia: Uchaguzi wa Marekani: Rais Joe Biden ampisha Kamala Harris

Biden amekabiliwa na miito ya mara kwa mara ya kumtaka ajiondoe mbioni kutokana na maswali kuhusu umri wake mkubwa na uwezo wa kiakili. Hii ilichochewa na namna Biden alivyofanya vibaya katika mdahalo wa televisheni dhidi ya Trump wiki tatu zilizopita. Harris anatarajiwa kupata uungaji mkono rasmi kutoka kwa wajumbe katika Mkutano Mkuu wa chama cha Democratic mjini Chicago mwezi ujao. Tangazo la Biden kumuidhinisha Harris lina uzito mkubwa wa kisiasa. Lakini, hana mamlaka ya kuwalazimisha wajumbe kumpigia kura aliyempendekeza.