1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden amshambulia Trump na Waripublican

Hawa Bihoga
8 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ametumia hotuba ya hali ya taifa kulaumu kile alichokiita hotuba za chuki, kisasi na uchochezi kutoka kwa mwanasiasa na mtangulizi wake Donald Trump, akitaja zinahatarisha uhuru duniani.

Picha yakutengeneza ikimonesha Rais wa Marekani Joe Bidenna mtangulizi wake Donald Trump.
Picha iliowekwa pamoja ya rais wa Marekani Joe Biden na upande mwingine ni mtangulizi wake Donald TrumpPicha: ABACA/IMAGO;AP Photo/picture alliance

Katika hotuba yake mbele ya Bunge, rais Joe Biden ambae yupo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi kuwania muhula mwingine wa uongozi, alitumia takriban dakika 68 kumshambulia mtangulizi wake na mwanasiasa Donald Trump ambae hamkutaja moja kwa moja kwa jina, kadhalika akitumia muda mwingi kutuliza wasiwasi juu ya umri wake na utendaji kazi.

Rais Biden alihusisha hatua ya Trump kusifu watu waliovamia bunge katika jaribio la kuzuwia matokeo ya uchaguzi wa 2020 na vitisho dhidi ya demokrasia nje ya nchi, na kusema uhuru na demokrasia ya Marekani vilikuwa vinashambuliwa kutokae ndani na nje.

Biden aliyasema hayo huku pia akilisihi bunge kuunga mkono juhudi za Ukraine kujilinda dhidi ya vita vya uvamizi wa Urusi vilivyodumu kwa miaka miwili sasa.

Alisema Ukraine inaweza kumuzuwia Putin ikiwa marekani itasimama nayo na kuipatia silaha inazohitaji kujilinda.

"Sasa mtangulizi wangu, rais wa zamani wa Republican, anamuambia Putin fanya kila unachotaka. Hiyo ni nukuu. Rais wa zamani wa Marekani kiukweli alisema hivyo, akimnyenyekea kiongozi wa Urusi. Nadhani hii inaghadhabisha. Ni hatari. Na haikubaliki." Sehemu ya hotuba ya Biden ilisema.

Hotuba ya hali ya taifa ndiyo tukio muhimu la usiku katika kalenda ya ikulu ya White House ikiwapa marais fursa ya kuzungumza moja kwa moja na hadhira ya wabunge na watu mashuhuri katika ukumbi wa bunge na makumi ya mamilioni ya watazamanji wanaofuatilia kutoka nyumbani, ikiwa ndiyo hadhira kubwa zaidi ya Biden kwa mwaka huu.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwasilisha hotuba ya hali ya taifa.Picha: CHIP SOMODEVILLA/AFP/Getty Images

Rais huyo alijua angetazamwa siyo tu kwa ajili ya ujumbe wake, lakini pia ikiwa angeweza kuuwasilisha kw anguvu na ari.

Wasaidizi walisema Biden alikuwa na lengo la kuwathibitisha wanaomtilia shaka kuwa yuko imara na kuonyesha misimamo ya Warepublican anayoamini haiendani na wakati wa sasa wa nchi hiyo, hasa kuhusu suala la upatikanaji wa huduma za uavyaji mimba, lakini pia sera ya kodi na huduma za afya.

Biden asifu mafanikio katika awamu yake ya uongozi

Akisifu mafanikio yake ya kisheria, ikiwa ni pamoja na ufadhili wa kuimarisha utengenezaji wa chip za kompyuta kote nchini, Biden aliachana na maandishi yake yaliyotayarishwa ili kuwakosoa Warepublican ambao walipiga kura dhidi ya sera kama hizo lakini mwisho wa siku wanapata sifa kutokana na sera hizo kwenye maeneo yao ya uwakilishi.

Rais Biden alikuwa akizungumza mbele ya bunge ambalo limevunja rekodi ya kukosa ufanisi. Katika Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Republican, Spika Mike Johnson alichukua mamlaka miezi mitano iliyopita baada ya kuondolewa kwa spika wa zamani Kevin McCarthy.

Wabunge bado wanapambana kuidhinisha miswada ya ufadhili kwa mwaka huu na wamekwama kwa miezi kadhaa kuhusu miswada ya msaada wa kigeni ili kuisaidia Ukraine kuzuia uvamizi wa Urusi na kuunga mkono vita vya Israel dhidi ya Hamas.

Putin na Biden wakutana

01:15

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW