1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden amualika Zelenskiy

11 Desemba 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amemualika Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine katika Ikulu ya White House kujadiliana vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na umuhimu wa Marekani kuendelea kuisaidia nchi hiyo.

Ukraine | Unabhängigkeitstag in Kiew | Wolodymyr Selenskyj
Rais Volodymyr Zeleskiy wa Ukraine kuwasili Marekani siku ya Jumatatu (Disemba 11).Picha: kyodo/dpa/picture alliance

Taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili (Disemba 10) na Ikulu hiyo ilisema viongozi hao wawili wangelizugumzia mahitaji muhimu ya Ukraine kwa sasa.

Mkutano huo wa Jumanne (Disemba 12) unafanyika wakati serikali ya Biden ikijaribu kufikia makubaliano na bunge yatakayoruhusu msaada wa kijeshi kwa Ukraine na Israel.

Soma zaidi: Zelensky ameonya dhidi ya kusambaratika kwa ushirikiano wa mataifa ya Magharibi

Ofisi ya Rais Zelenskiy imesema kiongozi huyo angeliwasili mjini Washington siku ya Jumatatu (Disemba 11), tayari kwa vikao kadhaa vya mikutano na majadiliano.

Mbali na mkutano wake na Biden, Zelenskiy alipangiwa pia kukutana na maseneta kwenye jengo la bunge siku ya Jumanne, ambako angelikuwa na mazugumzo ya faragha na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW