1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden anaweza kurudisha ushirikiano wa kimataifa na uongozi?

9 Novemba 2020

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameapa kuondokana na sera ya nchi kujichukulia maamuzi. Lakini ili kuweza kurejesha uongozi wa Marekani atahitaji kurejesha Imani ya washirika waliotengwa na kuwawajibisha wapinzani. 

Deutschland Protest gegen die Wahl von Donald Trump in Berlin
Picha: John Mcdougall/AFP

Biden ameapa kurejesha jukumu la uongozi wa Marekani duniani kwa kuibatilisha sera ya kujichukulia hatua kwa upande mmoja iliyowekwa na utawala wa Trump na kuangazia upya miungano ya muda mrefu ya kimataifa. Anasema serikali yake itaboresha diplomasia na kuongoza kwa kile alichokiita "nguvu ya mfano” na sio "mfano wa nguvu.”

Biden amerithi hali ambayo washirika wanahoji uadilifu wa Marekani, huku mahusiano kati ya Marekani na madola mengine ulimwenguni yakiwa mabaya.

Rais mteule ameapa kurekebisha uharibifu huo kadri inavyowezekana katika siku zake za kwanza 100 madarakani kwa kubatilisha amri kadhaa zilizosainiwa na Rais Donald Trump. Amri hizo zilisitisha makubaliano ya kimataifa na miungano ambayo rais alidai haikuwa ya haki kwa Marekani kutokana na sababu mbalimbali. Wakosoaji wanasema hatua hizo hazikuleta tija na kujitenga kwa Marekani kuliiruhusu China kuutanua uwepo wake kutokana na pengo la Marekani. Hizi hapa baadhi ya sera za kigeni ambazo rais huyo mteule ameapa kuzibatilisha mara moja:

Mkataba wa Nyuklia wa Iran

Mataifa yaliyosaini mkataba wa nyuklia wa Iran yameahidi kuunusuru licha ya Marekani kujiondoa chini ya TrumpPicha: picture-alliance/Xinhua/Guo Chen

Trump kila mara aliupinga mkataba wa nyuklia wa Iran akisema ni moja ya mikataba mibaya kabisa katika historia na akaiondoa Marekani mnamo Mei 8 2018. Pia alirejesha vikwazo dhidi ya Iran na yeyote anayefanya biashara nayo.  Ulisainiwa na China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, Ujerumani na Iran chini ya utawala wa Obama mwaka wa 2015.

Soma pia:Marekani yataka Iran iwekewe upya vikwazo

Biden anasema sera ya Trump haifai na ilitumika tu kuongeza mivutano. Ameahidi kurejea katika mkataba wa nyuklia, lakini anasema ataondoa tu vikwazo baada ya kuthibitishwa kuwa Iran inaheshimu kikamilifu kanuni za mkataba huo.

Biden pia huenda akatafuta kujitenga na adui wa kikanda wa Iran na mshirika wa Uarabuni mkubwa wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Saudi Arabia. Biden anaweza kufanya hivyo kwa kusitisha msaada wa Marekanikwa vita vya Saudia nchini Yemen.

Makubaliano ya Tabia nchi ya Paris

Biden, alichaguliwa kwa sehemu kutokana na ahadi yxake ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, amerudia mara nyingi kusema kuwa atarejea mara moja katika Makubaliano ya Paris ya Tabia nchi. Trump, aliiondoa Marekani katika mkataba huo Juni 1, 2017, akidai unaipendelea China.

Biden ameahidi kujenga uchumi wa nishati safi ili kugharamia miradi ya kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)

Chini ya Trump, Marekani imejichukulia maamuzi ambayo yamekosolewaPicha: Reuters/Prime Minister's Office/A. Scotti

Utawala wa Biden umeahidi kurejea haraka katika WHO na kuomba kuongoza juhudi za taasisi hiyo za kupambana na janga la corona. Marekani ilikuwa na ushawishi mkubwa katika shirika hili muhimu la afya ya umma, kwa kuchangia asilimia 15 ya bajeti yake (Ujerumani huchangia asilimia 5.6). Julai 7, 2020, Rais Trump alitangaza kuwa Marekani inajiondoa katika shirika hilo – ambalo miongoni mwa mambo mengine linaratibu majaribio ya chanjo ulimwenguni – kuanzia Julai 6, 2021.

Umoja wa Mataifa

Trump alitishia kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, ijapokuwa mpaka sasa Marekani imejiondoa katika mashirika mawili tu ya taasisi hiyo: Baraza la Haki za Binaadamu – UNHRC na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO. Marekani ilitaja kudhulumiwa kwa mshirika wake Israel katika mashirika hayo.

Biden anaiunga mkono Israel na alikaribisha makubaliano ya karibuni ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, lakini utawala wake huenda utashinikiza kusitishwa ujenzi Israel wa makaazi ya na unyakuzi pamoja na kupaza sauti zaidi kuhusu mahitaji ya Wapalestina katika Umoja wa Mataifa.

WTO, NATO na Seneti

Masuala mengine Biden atapaswa kuyashughulikia ni hadhi ya mahusiano ya biashara pamoja na ndani ya taasisi kama vile Shirika la Biashara Ulimwenguni – WTO. Atalenga kurekebisha mahusiano na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kuimarisha ushirikiano, lakini malengo ya sera za kigeni yatabakia pale. Soma pia: Trump aziwashia moto nchi za NATO

Swali ni kama Biden anaweza kurejesha Imani na kufanikiwa alichokisema kwenye malengo yake: "Kuendeleza usalama, ustawi, na maadili ya Marekani kwa kuchukua hatua za dharura kuweka upya demokrasia yetu na miungano, kulinda mustakabali wetu wa kiuchumi, na kwa mara nyingine kuiweka Marekani katika nafasi ya mbele mezani, kuuongoza ulimwengu katika kuziangazia changamoto za dharura za kimataifa” – au kama ulimwengu umeshasonga mbele kwa miaka mine iliyopita.

DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW