Biden asema kuisaidia Ukraine ni jukumu la ulimwengu mzima
26 Januari 2023Biden amesema kuisaidia Ukraine kupambana na uvamizi wa Urusi na kulinda uhuru wake ni jukumu la ulimwengu mzima.
''Tangazo la leo linatokana na kazi kubwa na jukumu la mataifa kote ulimwenguni, yakiongozwa na Marekani kuisaidia Ukraine kulinda uhuru wa nchi yake. Na hii ndio maana yake.. kuisaidia Ukraine kutetea na kuilinda ardhi yake. Sio kitisho cha kuishambulia Urusi. Hakuna kitisho cha kuishambulia Urusi. Ikiwa wanajeshi wa Urusi watarudi kwao, basi watakuwa mahali wanakostahili. Na hivi vita vingekuwa vimekwisha.'' alisema Biden.
Kulingana na maafisa wa ngazi ya juu, Marekani itapeleka vifaru 31 chapa Abrams M1, hatua iliyohitimisha mabishano ya miezi kadhaa ndani ya serikali ya Biden kwamba ni vigumu kwa wanajeshi wa Ukraine kuvitumia na kuvitunza vifaru hivyo.